Naibu Waziri wa Nishati: Mgawo wa umeme nchini utaisha mwezi wa tatu
"Tuliahidi mwezi huu tuna ratiba ya kuzindua mtambo huu na ratiba hii iko palepale, tunawashukuru sana Watanzania kwa kuendelea kutuvumilia, matumizi ya umeme yanategemeana tukizalisha mwezi huu mgao utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunazalisha megawati 235 na mwezi wa tatu tutazalisha megawati 235 hivyo zitakuwa megawati 470 uhakika ni kwamba kufikia mwezi wa tatu mgao wa umeme utaisha nchini," - Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

Post a Comment