Mwenyekiti CCM Kinondoni ashiriki mazishi Wazo
Mwkt wa Wilaya ya Kinondoni Ndg Shaweji A. M. akiwa na Wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya sambamba na Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima aliyetokea bungeni Dodoma kuja kushiriki mazishi ya mke wa Mwenyekiti wa CCM WAZO A.M. Mbondela leo Trh 12/02/2024 kwenye Makaburi ya Salasala mwisho wa LamiI.
Mwenyekiti WA CCM WILAYA YA KINONDONI NDG. SHAWEJI akitoa Salam za rambirambi pia amesifu Wananchi kwa kujitokeza kumlaki mfiwa pia wanaCCM kujitokeza kwao kwa uwingi, umemfurahisha kwa kuona mahusiano yaliyopo Kati ya Chama na Wanachama, sambamba na Wananchi kwa ujumla.
Miongoni mwa Viongozi WA WILAYA ndani ya CCM, alikuwepo KATIBU WA CCM WILAYA ya KINONDONI, Mwenyekiti WA JUMUIYA ya WAZAZI WILAYA YA KINONDONI na Wajumbe wengine WA Kamati ya Siasa pia Wajumbe WA Halmashauri Kuu ya WILAYA.

Post a Comment