Kanisa la Lakewood: Mwanamke mwenye silaha auawa katika ufyatulianaji risasi mkubwa wa kanisa la Joel Osteen Texas

 


Mwanamke aliyekuwa amevalia koti na kuandamana na mtoto alifyatua risasi katika kanisa kuu la Texas lililokuwa na watu wengi kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa usalama, maafisa wanasema.

Mshukiwa huyo, aliyetajwa na polisi kuwa Genesse Ivonne Moreno, 36, alikuwa na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka saba, ambaye alijeruhiwa vibaya katika ufyatulianaji risasi wa Houston.

Wachunguzi walisema bunduki yake ilikuwa imeandikwa "Palestina" waligundua maandishi ya chuki dhidi ya Wayahudi.

Lakini walisema nia yake haiko wazi.

Mwanamume mwenye umri wa miaka 57 alipigwa risasi kwenye nyonga wakati wa kisa hicho na tangu wakati huo ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Mtoto wa mwanamke mwenye bunduki ambaye jina lake halikutajwa alipigwa risasi kichwani wakati wa ufyatulianaji risasi na kwa sasa "anapigania maisha yake", polisi walisema.Haijabainika ni nani aliyempiga risasi kijana huyo.

No comments