Msikisuse chama kwa kukosa nafasi za uongozi--Mlao
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani ndugu *Mwinshehe Mlao* amewataka wanachama wa CCM kutokisusa Chama hicho pindi wanapokosa nafasi za uongozi wakati wa chaguzi mbalimbali.
Hayo yamesemwa Leo tarehe *07/02/2024* Katika ziara ya Kamati ya Siasa tarafa kwa tarafa katika Mkutano wa Viongozi, wanachama na wananchi uliofanyika katika Kata ya Kirongwe Wilaya ya Mafia.
*Mlao* amesema kila mwanaccm ana wajibu wa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijijini na Vitongoji na si vinginevyo.
Aidha ameendelea kusema wanachama wanapaswa kufanya kazi ya ziada ya kuwashawishi wasio wanachama kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi wakati na baada ya uchaguzi.
Amehitimisha kwa kutoa nafasi kwa wa CCM kutoa kero ambazo zao na baadhi yake zimetatuliwa papo hapo na nyingine wamekabidhiwa wahusika kwa ajili ya kuzitafutia majibu.
Taarifa hii imeandaliwa na
David Mramba
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM
Mkoa wa Pwani.

Post a Comment