Mahakama ya juu zaidi ya Ecuador yahalalisha mauaji ya huruma

 


Ecuador imekuwa nchi ya pili katika Amerika Kusini baada ya Colombia kuhalalishamauaji ya huruma.

Mahakama yake ya kikatiba ilipiga kura saba hadi mbili kuunga mkono kuruhusu madaktari kumsaidia mgonjwa kufariki.

Mahakama ilisema uhalifu wa mauaji hautatumika tena kwa wanaofanya kazi ili kuhifadhi haki ya maisha yenye heshima.

Kesi hiyo ililetwa na mwanamke anayeugua ugonjwa wa mishipa ya fahamu unaojulikana kwa jina la ALS.

Alikuwa ameiambia mahakama mnamo Novemba kwamba alikuwa akipitia maumivu, upweke na ukatili, na alitaka kupumzika kwa amani.

Kanisa Katoliki la Kirumi, ambalo raia wengi wa Ecuador ni wafuasi wake, bado linapinga kwa dhati mauaji ya huruma.

Colombia iliharamisha mauaji ya huruma mwaka wa 1997.

Mgonjwa wa ALS Paola Roldán, ambaye yupo tu kitandani, aliwasilisha kesi yake mwezi Agosti, shirika la habari la AFP linaripoti.

Amyotrophic lateral sclerosis (ALS) ni aina ya kawaida ya ugonjwa wa neurone ya motor, hali isiyo ya kawaida ambayo huharibu sehemu za mfumo wa neva hatua kwa hatua, na kusababisha udhaifu wa misuli, mara nyingi kwa uharibifu unaoonekana.

Bi Roldán alipinga kifungu cha kanuni ya adhabu ambacho kilifanya mauaji ya huruma kuwa uhalifu wa mauaji na kuhukumiwa kifungo cha kati ya miaka 10 na 13 jela, AFP inasema.

"Nataka kupumzika kwa amani," aliambia kikao cha mahakama mwezi Novemba kupitia video. "Ninachopitia ni uchungu, upweke na ukatili."

Mahakama iliamua kwamba "haitakuwa jambo la busara kuweka wajibu wa kubaki hai kwa mtu ambaye anapitia hali hii".

“Kila binadamu anaweza kufanya maamuzi huru na yenye taarifa sahihi pale maendeleo yake binafsi yanapoathiriwa ambayo... ni pamoja na chaguo la kukomesha mateso makali yanayosababishwa na jeraha kubwa lisiloweza kurekebishwa la mwili au ugonjwa mbaya na usiotibika,” ilisema.

Baada ya uamuzi huo, Bi Roldán aliwaambia waandishi wa habari kwamba nchi yake imekuwa "yenye kufikiria wanayopitia wengine, huru na heshima zaidi".

"Vita vya haki za binadamu kamwe sio jambo lililonyooka kila wakati," aliongeza.

Babake Francisco Roldán aliwaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa na hisia tofauti kwa sababu wakati Paola aliweza kufikia "tukio la kihistoria" na "urithi kwa jamii ya Ecuador" familia yake ilikuwa na "moyo uliovunjika kwa sababu kunaweza kuwa na athari ... kifo cha binti yangu".

"Tunamuunga mkono Paola," alisema.

Mswada kuhusu mauaji ya huruma sasa itabidi umeandikwa na kuidhinishwa na Bunge, mchakato ambao unaweza kuchukua miezi mingi, lakini wakili wa Bi Roldán, Farith Simon alisema kuwa uamuzi huo "unaweza kutekelezeka mara moja".


No comments