Mike Iron Tyson, Evander wakutana baada ya miaka 27
Hatimaye Mike BondiaTyson na Evander Holyfield wameonesha kuwa hawana tofauti na wamedhihirisha kuwa sasa kuwa imani ipo kati yao baada ya kupozi kwenye picha ya pamoja, ikiwa ni miaka 27 tangu pambano lao lifanyike ambapo katika pambano hilo Bondia Tyson alimng’ata sikio Evander na kupelekea kupoteza pambano hilo mwaka 1997.
Baada ya pambano hilo, imepita miaka mingi sasa kukiwa na hali ya kutokuelewana kati yao lakini picha hiyo ya pamoja imeonesha kufuta tofauti zao za muda mrefu.
Inakumbukwa kuwa Tyson ndiye aliyemng'ata sikio Holyfield kwa mshtuko lakini alitupwa nje na mwamuzi Mills Lane. Hata hivyo, Tyson alipomng’ata tena sikio mpinzani wake, mara moja alienguliwa na kusababisha tukio hilo baya ulingoni huku akiambulia kupoteza pambano hilo.
Credit: TBConline

Post a Comment