Cristiano Ronaldo mwanamichezo aliyelipwa zaidi mwaka 2023


Cristiano Ronaldo alikuwa tayari ni miongoni mwa wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani kabla hajatimkia Saudi Arabia, ambako mshahara wake umemfanya aendelee kuwa juu kileleni kwa kukunja mkwanja mrefu hadi sasa.

Mwanasoka huyu Mreno amekuwa katika vita vya muda mrefu wa uchezaji wake wa soka na hasimu wake kutoka Argentina, Lionel Messi ambaye ameshinda mataji mengi ya mwanasoka bora duniani kuliko yeye, lakini angalau sasa anaweza kujipooza na ukwasi wa kutosha.



Katika orodha mpya iliyotolewa juu ya wanamichezo 100 wanaolipwa vizuri zaidi duniani, Ronaldo amekamata nambari moja, huku mshindani wake, ambaye ni mshindi wa Kombe la dunia, akiichezea Inter Miami ya Marekani, Lionel Messi, akiwa hata hayupo nafasi ya pili, badala yake nafasi hiyo inashikwa na mcheza Golf, John Rahm.

Kwa mujibu wa orodha mpya kutoka Sportico, Ronaldo alikusanya jumla ya paundi milioni 218, sawa na dola milioni 275, ambayo inahusisha mshahara wa pauni milioni 175 anazochukua kwa mwaka katika klabu yake ya Al Nassir, pauni milioni 45 kupitia mikataba ya matangazo na kampuni mbalimbali kama vile Nike, Herbalife, Armani, Tag Heuer, DAZN na PokerStars, achilia mbali brandi yake binafsi ya CR7.


Rahm, raia wa Hispania, anafuatia kwa kuchukua pauni milioni 144 kama mapato yake mwaka jana, ikiwa ni baada ya kutwaa taji la Masters 2023, kabla ya kuondoka na kusajiliwa na ligi inayofadhiliwa na Saudia ya Liv Golf ambao wanaaminika watamlipa kiasi cha pauni milioni 400.

Messi anafuata katika nafasi ya tatu kwa kulipwa kiasi kikubwa cha fedha kwa mwaka jana, akiwa ni miongoni mwa wanasoka watano waliopo katika Top Ten ya orodha hiyo ndefu ya wananmichezo mia moja, akiwa mbele ya wachezaji wenzake wawili wa zamani klabuni PSG, Kylian Mbape, na Neymar Jr.

2023's HIGHEST-PAID ATHLETES 

1. Cristiano Ronaldo (football) - £218m

2. Jon Rahm (golf) - £161m

3. Lionel Messi (football) - £103m

4. LeBron James (NBA) - £99.8m

5. Kylian Mbappe (football) - £99.2m

6. Neymar (football) - £96m

7. Stephen Curry (NBA) - £78.5m

8. Giannis Antetokounmpo (NBA) - £70.2m

9. Kevin Durant (NBA) - £69m

10. Patrick Mahomes (NFL) - £66.9m

11. Lamar Jackson (NFL) - £65.5m

12. Karim Benzema (football) - £61m

13. Rory McIlroy (golf) -  £61m

14. Tiger Woods (golf) -£61m

15. Max Verstappen (F1) - £59.5m

16. Shohei Ohtani (baseball) - £55.6m

17. Canelo Alvarez (boxing) - £52.4m 

18. Erling Haaland (football) - £50m

19. Lewis Hamilton (F1) - £49.2m

20. Max Scherzer (baseball) - £48.2m

21. Damian Lillard (basketball) - £47.8m

22. Klay Thompson (basketball) - £47.7m

23. Mohamed Salah (football) - £44.4m

24. Anthony Joshua (boxing) - £43.6m

25. Russell Westbrook (basketball) - £42.8m

26. Nick Bosa (NFL) - £42.5m

27. Viktor Hovland (golf) - £41.5m 

27. Scottie Scheffler (golf) - £41.5m

29. James Harden (basketball) - £40.9m

30. Joe Burrow (NFL) - £40.9m

31. Paul George (basketball) - £40.5m

32. Bradley Beal (basketball) - £40.1m

33. Kawhi Leonard (basketball) - £39.7m 

34. Luka Doncic (basketball) - £39.4m

35. Jimmy Butler (basketball) - £38m

36. Daniel Jones (NFL) - £37.7m

37. Jake Paul (boxing) - £37.3m

38. Joel Embiid (basketball) - £37.1m  

39. Brooks Koepka (golf) - £37m

40. Deshaun Watson (NFL) - £36.9m 

41. Devin Booker (basketball) - £36.7m

42. Aaron Rodgers (NFL) - £36.4m 

43. Nikola Jokic (basketball) - £36.3m

44. Anthony Davis (basketball) - £36.1m

45. Dak Prescott (NFL) - £35.7m 

46. Novak Djokovic (tennis) - £35.6m 

47. Trae Young (basketball) - £35.5m

48. Justin Verlander (baseball) - £35.3m 

49. Aaron Judge (baseball) - £34.9m

50. Zach LaVine (basketball) - £34.7m

51. Cameron Smith (golf) - £34.3m 

52. Kyrie Irving (basketball) - £34.3m 

53. Jordan Spieth (golf) - £34m 

54. Gervonta Davis (boxing) - £33.7m

54. Kyler Murray (NFL) - £33.7m

56. Carlos Alcaraz (tennis) - £33.5m

57. Jamal Murray (basketball) - £32.5m 

58. Ryan Garcia (boxing) - £32.1m

58. Mike Trout (baseball) - £32.1m  

60. Donovan Mitchell (basketball) - £32m

61. Rudy Gobert (basketball) - £31.9m

61. Talor Gooch (golf) - £31.9m

63. Jayson Tatum (basketball) - £31.8m

64. Tyson Fury (boxing) - £31.7m

65. Rashan Gary (NFL) - £31.6m

66. Tobias Harris (basketball) - £31.2m

67. Chris Paul (basketball) - £30.5m

68. Ben Simmons (basketball) - £30.4m

69. Anthony Rendon (baseball) - £30.4m

70. Pascal Siakam (basketball) - £30.1m 

70. Russell Wilson (NFL) - £30.1m

70. Sadio Mane (football) - £30.1m

73. CJ McCollum (basketball) - £30.1m

74. Jrue Holiday (basketball) - £30m

75. Zion Williamson (basketball) - £29.8m

76. Gerrit Cole (baseball) - £27.7m 

76. Corey Seager (baseball) - £29.7m

78. Karl-Anthony Towns (basketball) - £29.5m

79. Carlos Correa (baseball) - £29.3m

79. Josh Allen (NFL) - £29.3m

81. Kristaps Porzingis (basketball) - £29.1m

82. Brandon Ingram (basketball) - £28.6m

83. Riyad Mahrez (football) - £28.5m

83. Robert Lewandowski (football) - £28.5m

85. Chris Lindstrom (NFL) - £28.4m

86. Dustin Johnson (golf) - £28.3m

87. Khris Middleton (basketball) - £28m

88. Kevin de Bruyne (football) - £27.8m

89. Michael Porter Jr. (basketball) - £26.9m

90. Orlando Brown Jr (NFL) - £26.8m

91. Gordon Hayward (basketball) - £26.7m

92. Stephen Strasburg (baseball) - £26.6m 

93. Shai Gilgeous-Alexander (basketball) - £26.6m

94. Bryce Harper (baseball) - £26.3m

95. Kirk Cousins (NFL) - £26.2m

96. De'Aaron Fox (basketball) - £26.1m

97. Miguel Cabrera (baseball) - £26m

98. Bam Adebayo (basketball) - £25.9m

99. Giancarlo Stanton (baseball) - £25.8m 

100. Derek Carr (NFL) - £25.8m 

 

No comments