Katibu CCM Mbinga ashiriki Party Caucus cha Madiwani

 

Katibu wa chama Cha mapinduzi-CCM wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Comrade BASHIRU MADODI leo February 7-2024 ameshiriki kikao Cha *party caucus Cha madiwani wa chama hicho kutoka Halmashauri ya Mbinga Mji, kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa CCM Mbinga mjini.

Katibu MADODI ametumia wasaa huo kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani hao hususani, uwezo wa kuibua vipaumbele sahihi vya miradi ya Maendeleo ya wananchi na ubunifu wa kuongeza Mapato ya Halmashauri hiyo inayotegemea zaidi mapato kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ushuru wa mazao na sekta ya Biashara,

Taarifa hii imetolewa na Idala ya itikadi Uenezi na Mafunzo ya Chama Cha mapinduzi-CCM wilaya ya Mbinga

No comments