DIRA YA TAIFA NA MFUMO WA ELIMU NCHINI NI KAMA KULWA NA DOTO
Na Associated Dr.Mwampogwa-Tanga.
Taifa linapokuwa na Dira yake aidha ya miaka 50 au 100 ijayo ni lazima taifa hilo lihakikishe kuwa Mfumo wake wa Elimu unasadifu na Dira yake ya nchi lengo ni kurahisisha utekelezaji wa Dirá hiyo.
Tunapokuwa na Mfumo wa Elimu unaosadifiana na Dira yetu ya nchi tafsiri yake Mfumo wetu utatuzalishia Wataalam ambao wanahitajika katika kuhakikisha Dira hiyo inatekelezwa kwa kiwango kilicho Bora na kilicho kusudiwa.
Kuna hatari kubwa sana iwapo Dirá ya nchi itakosa mahusiano na Mfumo wa Elimu tafsiri yake nchi itazalisha Wataalam wengi sana tena huenda wakawa wazuri sana lakini wakashindwa kusaidia kuendesha Dira ya nchi yao maana Wataalam hao hawasadifiani na Dira ya nchi.
Mfano wa kawaida sana Shule moja ya Sekondari inaweza kuwa inahitaji Walimu 25 na ukienda katika Shule hiyo ukakuta kuna Walimu 50 na bado ukaambiwa ina Uhaba mkubwa wa Walimu kwanini? Shule hiyo huenda ilihitaji Walimu 15 wa Masomo ya Sanaa na Walimu 10 wa Masomo ya Sayansi Jumla 25.Lakini tukajikuta katika Shule hiyo tuna Walimu 46 wa Masomo ya Sanaa na Walimu 4 wa Masomo ya Sayansi Jumla 50 hivyo pamoja na wingi wa Wataalam (Walimu) hao lakini haujasaidia kutatua tatizo maana tuna wingi usio hitajika.Ahsanteni.
Hivyo tunapotengeneza Dira ya nchi yetu tusisahau kuweka mazingira ya kuandaa Rasilimali Watu,Vitu nk katika kuhakikisha hatukopi Wataalam hatukwami katika Safari yetu.

Post a Comment