BASHUNGWA AAGIZA WAHANDISI KUONGEZEWA WIGO

 


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) kuongeza wigo wa kuwajengea uwezo Wahandisi Washauri nchini ili kuhakikisha utalaam na ujuzi unakuzwa kwa maendeleo ya nchi.

Bashungwa amezungumza hayo jijini Dodoma katika mkutano uliokutanisha Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), na kusisitiza kuweka mikakati mahususi ya uendelezaji wa Wahandisi Washauri kitaaluma ili kukuza tasnia ya Uhandisi.

“Vipaumbele na maagizo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika sekta hii ni kuona ushiriki mkubwa wa Wahandisi na Makandarasi Wazawa katika kazi za ujenzi na usimamizi wa miradi (Local Content), sisi kama wasaidizi wake tuhakikishe tunalitekeleza hili”, amesema Bashungwa.

Aidha, ameelekeza kuhakikisha kunakuwa na uwepo wa ushirikishwaji wa Wahandisi wahitimu katika mpango wa mafunzo kwa vitendo (SEAP) kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa nchini ili kuwajengea uwezo.

Vilevile, ameagiza kuangalia maeneo yote yenye changamoto katika Sheria ya Usajili ili kuwawezesha wahandisi kufanya ubunifu na kusaidia nchi katika uchumi wa viwanda na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

No comments