ECOWAS yaelezea wasiwasi wake kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi wa Senegal
Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi ECOWAS imeelezea wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa mamlaka ya Senegal kuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 25 Februari 2024.
Wanasiasa wa upinzani nchini humo wameitaja hatua hiyo kuwa ni mapinduzi ya kikatiba.
Katika tangazo lililoshangaza nchi, Rais Mackey Sall alisema kuwa sababu ya hatua yake hiyo ni orodha ya wagombea katika chaguzi zilizopangwa. Wengi wa wagombea wamezuiwa kugombea.
Katika taarifa yake Jumamosi usiku huko Abuja, Makao Makuu ya ECOWAS yalihimiza wanasiasa nchini kutanguliza mazungumzo na ushirikiano kwa ajili ya uchaguzi wa uwazi, jumuishi na wa kuaminika.
Viongozi wa kambi ya kikanda pia walitoa wito kwa "mamlaka zinazofaa kuharakisha michakato mbalimbali," ili kupanga tarehe mpya ya uchaguzi.
"Tume ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi imezingatia uamuzi wa mamlaka ya Senegal kuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 25 Februari 2024," taarifa hiyo ilisema.
Kambi hiyo imempongeza zaidi Rais wa Senegal, Macky Sall kwa kuendelea na uamuzi wake wa awali wa kutogombea muhula mwingine na kumtaka aendelee kutetea na kulinda mila ya kidemokrasia ya muda mrefu ya nchi hiyo.Tangazo la Rais Sall lilizua hali ya wasiwasi nchini humo.
Chini ya kanuni za uchaguzi nchini, angalau siku 80 lazima zipite kati ya kuchapishwa kwa amri hiyo na uchaguzi, ambayo ina maana kwamba mapema zaidi inaweza kufanywa ni mwishoni mwa Aprili.Senegal haijawahi kuchelewesha kura ya urais.

Post a Comment