Wahouthi waapa kujibu mashambulizi ya Marekani na Uingereza
Waasi wa Houthi wameapa kujibu mashambulizi ya Marekani na Uingereza baada ya mashambulizi kadhaa dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya meli zinazopitia Bahari Shamu.
Msemaji wa kundi la waasi alisema katika awamu hii ya tatu ya mashambulio ya pamoja ya Uingereza na Marekani hayatawazuia kutoka kwenye "msimamo wao wa kimaadili, kidini na wa kibinadamu" wa kuunga mkono Wapalestina.
Wahouthi wamekuwa wakishambulia meli za kibiashara katika Bahari Shamu tangu Novemba. Takriban 15% ya biashara ya kimataifa hupitia Bahari ya Shamu kila mwaka, yenye thamani ya zaidi ya $1tn (£790bn).
Mashirika mengi ya meli yameanza kuepuka eneo hilo na yanatumia njia ndefu zaidi kuzunguka kusini mwa Afrika badala yake.
Kulingana na Houthis, mashambulizi 48 yalifanyika katika muda wa saa chache na kulenga mji mkuu Sana'a pamoja na maeneo mengine kote nchini.
Bado hakuna majeruhi walioripotiwa.Katika taarifa ya pamoja, Marekani, Uingereza na nchi nyingine zinazounga mkono operesheni hiyo zilisema awamu ya tatu ya mashambulizi yaligonga "malengo 36 ya Houthi katika maeneo 13 nchini Yemen".

Post a Comment