Willy Isangura afariki dunia leo
Bingwa wa uzito wa juu wa ngumi uzani wa kilo 100 Tanzania, aliyetamba katika miaka ya sabini na themanini, Willy Isangura, amefariki hospitali ya Muhimbili alfajiri ya leo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Chaurembo Palasa, Rais wa Kamisheni ya Ngumi Tanzania, bingwa huyo aliyeiletea Tanzania sifa katika michuano ya Jumuia ya Madola miaka hiyo, alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo.
Taarifa zaidi zitatolewa na familia ya Marehemu. Rest In Peace Isangura

Post a Comment