Dani Alves ahukumiwa miaka minne jela kwa ubakaji

 


Nyota wa zamani wa Brazil na Barcelona, Dani Alves, baba wa watoto wawili, leo asubuhi amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana katika choo cha klabu moja ya usiku nchini Hispania.

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye amekuwa akihifadhiwa rumande katika gereza la Brians 2 lililopo karibu na mji wa Catalan tangu alipokamatwa Januari mwaka jana, yupo huru kukata rufaa.

Mwanasoka huyo alikiri mahakjamani kufanya mapenzi na mwanamke huyo katika vyoo vya klabu ya usiku Sutton Desemba 30 mwaka juzi na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini akasisitiza kjuwa jambo hilo lilifanyika kwa makubaliano

.

Lakini mwanamke huyo ameiambia mahakama kwamba si kweli kuwa alikubaliana naye, isipokuwa mchezaji huyo raia wa Brazil, alimlazimisha.

Wakili wa Alves, Ines Guardiola - ambaye amethibitisha kuwa mteja wake atakata rufaa, akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama huko Barcelona.



No comments