Mazishi ya Kada wa CCM yaleta sintofahamu Kanisa Katoliki
Habari katika mitandao mbalimbali ya kijamii zinasema marehemu alipinga Waraka wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.
Ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangaza kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yao Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.
Lakini watu walipofika kanisani hapo, walikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.
Uamuzi wa haraka ulifanyika wa kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.
Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu, milango ya kanisa pia ilikuwa imefungwa, kiasi cha kupelekea familia kutafuta wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.
Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.
Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Post a Comment