Akaunti za kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Khamenei kwenye Facebook na Instagram zafutwa
Meta imesema ilifuta akaunti za Facebook na Instagram za Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, kwa kukiuka sera yake ya maudhui.
"Tuliondoa akaunti hizi kwa kukiuka mara kwa mara sera yetu ya Mashirika Hatari na Watu Binafsi," msemaji wa Meta aliambia AFP siku ya Alhamisi.
Ingawa Meta haikutaja vita vya Gaza, kampuni hiyo imekuwa chini ya shinikizo la kumpiga marufuku Khamenei tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7.
Baada ya shambulio hilo, Khamenei alitangaza kuunga mkono Hamas, lakini alikanusha kuhusika kwa Iran.
Pia alieleza hadharani uungaji mkono wake kwa "kulipiza kisasi kwa Wapalestina kwa shambulio la Israel huko Gaza, na kwa mashambulizi ya kundi la Houthi huko Yemen kwenye meli katika Bahari ya Shamu."
Khamenei ana wafuasi milioni tano kwenye Instagram.
"Katika jitihada za kuzuia madhara mashinani, haturuhusu mashirika au watu binafsi wanaotangaza ghasia au kushiriki vurugu kwenye majukwaa yetu," Meta ilisema katika uamuzi wake.
Pia ilisema "itaondoa utukufu, msaada na uwakilishi wa mashirika na watu binafsi hatari."
BBC

Post a Comment