Rais Samia amteua RAS mpya Iringa

 



Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Doris Kalasa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus leo, Alhamisi Januari 18, 2024 imeeleza kuwa Kalasa anachukua nafasi ya Mhandisi Leonard Robert Masanja aliyestaafu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kabla ya uteuzi huu, Kalasa alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais –Ikulu.

No comments