Pwani yaingia makubaliano na IFM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani imeingia mkataba wa makubaliano na Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) unaohusiana na masuala mbalimbali kwa lengo la kujenga mahusiano ya karibu baina ya ofisi hiyo na Chuo hicho.
Mkataba huo umesainiwa tarehe 17 Januari 2024 baina ya Rashid Mchatta Katibu Tawala Mkoa Pwani kwa Upande wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Profesa Josephat Lotto Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwa niaba ya chuo huku ukishuhudiwa na baadhi ya wataalam kutoka Sekretariet Mkoa pamoja na wataalam kutoka chuo cha Ofisi ya usimamizi wa fedha IFM.
Pia Mkataba huo utahusisha masuala ya kushirikiana katika nafasi za mazoezi kwa wanafunzi,nafasi ya utafiti kati ya taasisi hizi mbili ili kutatua matatizo ya kijamii, pamoja na kushirikiana katika ukusanyani wa takwimu mbalimbali kw ajili ya matumizi ya Mkoa .

Post a Comment