Katibu CCM misungwi atinga Kijima


Na King Bashite

Misungwi Mwanza


Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi  ikiongozwa na mwenyekiti wake na Katibu wa CCM wilaya ya Misungwi.Comrade  MWITA NYAINGI imefanya ziara kijiji cha Kijima kata ya Kijima kwa lengo la kuwapa pole wananchi wa kijiji hicho waliokumbwa na changamoto ya nyumba zao, mazao pamoja na mifugo kuharibiwa vibaya sana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha mwishoni mwa mwezi wa 12/2023.

Kaya zilikumbwa na changamoto hiyo ya kukosa makazi na shule moja ya msingi majengo yake mawili yalibomolewa na dhoruba hiyo. 

Katibu wa CCM Wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa Sekretarieti ya Halmashauri kuu ndugu Mwita pamoja na kuwasilisha Salamu za Chama, Amekabidhi Gunia 6 za Mahindi ambazo zimetolewa na Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Misungwi Ndugu Alexander pastory Mnyeti na kuwakabidhi wananchi hao ili waweze kugawana. 

Mheshimiwa Diwani kata ya Kijima Ezekiel Kanzaga na mwenyekiti wa kijiji cha Kijima na wananchi wote kwa pamoja wamempongeza Mheshimiwa mbunge kwa upendo alionao na kumshukuru sana  kwa kuonyesha upendo huo Toka siku ya kwanza tu ya tukio kuwafikia wananchi hao na pia wameushukuru sana uongozi wote wa chama cha mapinduzi (CCM). Kwa kuwa nao bega kwa bega.

Sekretarieti ya Chama cha Mapindunzi Wilaya imempongeza Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Misungwi Comrade PAUL CHACHA MATIKO (MSEMINARI)  na Mheshimiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Ndg Joseph Mafuru kwa hatua za haraka walizozichukua baada ya tatizo kutokea ikiwemo kutengwa kwa kiasi Cha shilingi Milioni 40 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule ya Msingi KIJIMA ambayo majengo yake yaliharibika. 

Misungwi ni yetu sote tushirikiane kuijenga. CCM ni chama chetu tunakupenda muda wote.

Mwisho katibu wa CCM Wilaya Misungwi amewataka wananchi kuwa na subira huku serikali inayoongozwa na Chama cha Mapindunzi ikiendelea na hatua nyingine za kuwasaidia 


No comments