ORODHA YA GOMES MSIMBAZI YAVUJA


Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na nje

WAKATI dirisha la usajili likikaribia kufunguliwa, tayari makocha wa timu kubwa wameanza kuvujisha orodha ya wachezaji wanaowahitaji kwa ajili ya msimu ujao.

Kocha Didier Gomes Da Rosa Simba anadaiwa kuwahitaji wachezaji kadhaa ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano ya ndani na ile ya kimataifa msimu ujao.

 Wachezaji walioainishwa kuwa anawataka washambuliaji wawili raia wa Congo, Dark Kabangu wa Dc Motema Pembe, Walter Bwalya wa Al Ahly na beki wa kati Idumba Fasika ambaye nae ni Mkongo anayekipiga katika klabu ya FC Lupopo.

 

 Ripoti hiyo pia imemtaja kiungo mshambuliaji

Anayo Iwuala raia wa Nigeria anayekipiga katika klabu ya kwao Enyimba Fc, Karim Kimvuidi Kiekie kiungo mshambuliaji raia wa Kongo anayekipiga katika timu ya DC Motema Pembe.

 Ripoti hiyo pia inamtaka beki wa kati wa Burundi, Fredrick Nsabiyumva anayekipiga katika klabu ya Chipa United, Khalid Aucho kiungo mkabaji raia wa Uganda anayekipiga Lel Makkasa na Last Jesi kiungo mshambuliaji raia wa Zimbabwe ambaye ni mchezaji huru.

Licha ya hivyo kuna baadhi ya wachezaji wataondoka kikosini humo ili kutoa nafasi kwa wachezaji hao wapya kuingia kikosini humo.

 

No comments