Mbowe akutana na Balozi wa Uingereza Nchini

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini, David Concar. 

Ubalozi wa Uingereza ambao ndiyo uliotoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa X, haikusema ni maeneo gani yalizungumzwa. Hata hivyo, huu umekuwa ni mfululizo wa kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini kufabnya mazungumzo na mabalozi wa nchi mmbalimbali nchini.

Ameshakutana na mabalozi wa nchi za Marekani, Ubeligiji, China na Brazil.

No comments