Maneno azikwa nyumbani kwake Chalibze
Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Marehemu Ramadhani Maneno kwa kipindi Cha 2017 hadi 2022 yamehitimishwa leo Alhamis Januari 4, 2024 saa saba na nusu mchana tarehe nyumbani kwake Chalinze.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Mhe, Daktari Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne.
Aidha Mhe, Daktari Samia Suluhu Hassan, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika msiba huo ametuma salamu za Rambirambi na kutoa ubani wa Shilingi milioni 10.
Taarifa hii imeandaliwa na
David Mramba
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM
Mkoa wa Pwani.

Post a Comment