Kashfa Kampuni Kubwa ya Bia

*Yadaiwa kuwa na mikataba miwili ya ajira. Mmoja wa Uongo wenye kuhadaa taasisi za Serikali ili kukwepa kodi, mwingine wa kweli unaolipwa kwa dola ya Marekani


Kampuni moja kubwa na maarufu nchini kwa utengenezaji, usambazaji na uuzaji wa vileo ikiwemo bia, inadaiwa kuwa na mikataba miwili kwa waajiriwa wake, wazawa na wa kigeni ikiwa na lengo la kukwepa kodi.


Kwa mujibu wa nyaraka ambazo blog hii imeziona kutoka taasisi moja kubwa ya ukaguzi wa mahesabu, kati ya Januari 2009 na Oktoba 2010 ilibaini upungufu mkubwa katika mikataba ya ajira, kodi ya zuio, kodi ya faida ya mapato ya kampuni, kodi ya ongezeko la thamani (VAT), ushuru wa biashara na kodi ya mapato yatokanayo na ajira (PAYE).


Hasa, taarifa inaonyesha ukwepaji kodi kwa kodi ya mapato yatokanayo na ajira tu ilifikia takribani $2.4 milioni kwa mwaka, hali ambayo iliendelea kwa miaka mingi tangu mwaka 2001 hadi 2010.


Mikataba ya wafanyakazi wandamizi inaonyesha kiasi cha fedha za Kitanazania, wakati orodha ya wapokea mshahara huonyesha kiasi tofauti kwa kulinganisa na kile kilichoko kwenye mikataba.


Uchunguzi unaonyesha kampuni hiyo ya vinywaji ilikuwa ikitumia aina mbili za mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kutoka nje ya nchi na wafanyakazi waandamizi ambao ni Watanzania. Aina moja ya mshahara (kurasa 3 tu) unaonyesha mshahara wa uwongo ambao ni wa chini katika shilingi za Tanzania – aina hii ya mikataba ndiyo hutumika kuwaonyesha maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kwa mchakato wa kupata kibali cha kazi, wakati aina nyingine ya  mkataba wenye ukurasa wa ziada (kurasa 4) ukionyesha mshahara kwa Dola za Kimarekani ukifichwa.

Ofisa mmoja wa kampuni hiyo alithibitisha ukaguzi wa mahesabu ya kampuni yaliyokwishakaguliwa ulifanyika tena kuanzia mwaka 2006 hadi 2010 na kuthibitisha ukaguzi uliofanywa na Kampuni mbili pacha zanye ofisi Tanzania na Kenya.


Taarifa ya ukaguzi ya taasisi hiyo ya ukaguzi ilikuwa kwa miezi 20 (mwaka 2009 hadi mwaka 2010) ambayo inaonyesha maeneo ambayo kodi ilikwepwa, ni nini kilitokea kuanzia mwaka 2001 hadi 2008? 

Blog hii inaendelea kufuatilia nyaraka zaidi za ukwepaji huo wa kodi


No comments