Spika Tulia aongoza kikao cha IPU

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza kikao cha Maspika na Wenyeviti wa Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola wakati wa uwasilishaji mada kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabia nchi katika Ukumbi wa Speke Resort Munyonyo nchini Uganda leo tarehe 4 Januari, 2023 
Mada hiyo ni sehemu ya Mkutano unaoendelea ambapo pamoja na mambo mengine Viongozi hao watajadili masuala ya jinsia na ushirikishwaji wa vijana pamoja na ujengaji wa misimamo ya pamoja ya kibunge.

No comments