Kashfa iliyomkumba TB Joshua inavyowatafuna manabii Tanzania
Na
Mwandishi Wetu
Wakati
dunia ikiwa bado haiamini kile kinachoendelea kuibuliwa na Shirika la
Utangazaji la Uingereza BBC, juu ya udanganyifu na hila zilizokuwa zikitumiwa
na TB Joshua, mmoja wa wahubiri aliyepata umaarufu mkubwa duniani, hali imekua
tete kwa watumishi wa Mungu wanaofanya shughuli zao nchini Tanzania.
BBC imefichua, kwa mara ya kwanza, jinsi
mwinjilisti wa televisheni wa Nigeria marehemu TB Joshua alivyoghushi miujiza
iliyovutia mamilioni ya watu kwenye kanisa lake.
Mhubiri huyo, ambaye anatuhumiwa kwa unyanyasaji
na utesaji ulioenea kwa takriban miaka 20 , alianzisha Kanisa lake la Synagogue
Church of All Nations (SCOAN) mjini Lagos zaidi ya miongo mitatu iliyopita.
Kuinuka kwake kwa umaarufu kulifungamanishwa kwa karibu na uwezo wake wa
kujidai wa kuwa na nguvu za kimungu na uwezo wake unaodhaniwa kuwa wa kuponya
wagonjwa.
Hapa Tanzania, wapo wahubiri ambao nao wamejipa uwezo huo
na kuwafanya kuwa na mamia kwa maelfu ya wafuasi. Baadhi ya watumishi hao wa
Mungu, kama alivyokuwa TB Joshua, wamekuwa wakifanya miujiza ya kuwainua watu
waliolala kwa kushindwa kutembea, kuponya magonjwa yaliyoshindikana na hata
kusaidia watu kupata vyeo makazini na mafanikio katika biashara zao.
Baadhi ya waumini hao waliozungumza na Ojuku Blog,
wameelezea kushtushwa kwao na taarifa za udanganyifu wa TB Joshua, kwani hata
mhubiri wao, alisema alipata nguvu za upako kutoka kwa mtumishi huyo raia wa
Nigeria.
“Kwa kweli inabidi tujitafakari upya. Hiki kinachotokea
Nigeria kinatupa tafakuri sana maana naona kama mambo yanafanana. Serikali
itusaidie kuchunguza huenda na sisi tunaibiwa bila kujijua,” anasema muumini wa
kanisa moja linaloshuhudia miujiza kila mwisho wa wiki katika kanisa
wanalosali, ambalo kwa sasa linahigadhiwa.
Mwanaharakati mmoja ambaye hataki jina lake litajwe,
anaiambia blog hii kuwa manabii wengi nchi hii ni wa uongo na kwamba
wanafanikiwa zaidi kutokana na wananchi wengi kukata tamaa na hivyo kujikuta
wakitaka kufanikiwa kwa njia za mkato.
“Wee hebu jiulize, anaonekana mwanamke ambaye hata
kiswahili tu hawezi, anasema mtoto wake alijisaidia kwa njia ya haja kubwa eti
sijui mjusi, nyembe na nini sijui. Sasa kule kijijini eti anapiga picha yupo
kwenye choo cha sinki, lakini ukimtazama, huamini kama hata anajua kutumia
smartphone. Ni utapeli tu umejaa,” anasema.

Post a Comment