Idadi ya waliofariki katika tetemeko la ardhi Japan yafika 62

Jengo la ghorofa nane likiwa limeanguka huko Wajima

Onyo la kutokea tsunami limeondolewa nchini Japan baada ya tetemeko kubwa la ardhi, lakini idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 62, huku nyumba zikiharibiwa.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amesema idadi ya waliojeruhiwa na kiwango cha uharibifu ni kikubwa.

Takribani watu elfu moja kutoka timu za uokoaji wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu wanaoaminika kukwama chini ya vifusi vya nyumba.

Jeshi la Japan linatoa vifaa vya msaada ikiwa ni pamoja na kusambaza maji, chakula na mablanketi.

Onyo la tsunami kando ya Bahari ya Japan limeondolewa, kumaanisha hakuna hatari tena ya tsunami.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema yuko tayari kutoa msaada unaohitajika kwa Japan.

No comments