Afcon 2023: Ivory Coast, Nigeria, Misri, Ghana na Senegal katika Kundi A, B na C
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 yataanza nchini Ivory Coast katikati ya Januari. Senegal itajitahidi kutetea taji lake.
Ni mashindano yenye muundo wa timu 24 - ikimaanisha timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu hatua ya mtoano, na timu nne za juu zilizo katika nafasi ya tatu zitaungana nao.
Fainali za mwisho za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon zilishuhudia: Comoro na Gambia zikifuzu huku Ghana, mabingwa mara nne, wakirejea nyumbani. Tutarajie nini katika mashindano haya ya 34?
BBC imezungumza na wachezaji, magwiji wa soka barani Afrika na waandishi wa habari kuyatathmini makundi A, B na C.
Kundi A
Linaundwa na Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea-Bissau. Nchi mwenyeji Ivory Coast ilitolewa na Nigeria, mshindi mara tatu wa mashindano hayo, na Equatorial Guinea, ilifanikiwa kufika robo fainali katika mashindano yaliyopita.
Guinea-Bissau, itajaribu kutinga hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.
“Kundi hili ni gumu sana,” anasema mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba – ambaye aliifungua timu hiyo magoli 65. "Timu zote zinastahili kufuzu na zitapambana.”
"Nigeria, ikiwa na Victor Osimhen na wachezaji wengine, ni timu kubwa. Nafikiri jambo kubwa litakuwa ni kuelekeza nguvu zetu kama Ivory Coast kwenye michezo yetu, timu yetu na kuiunga mkono timu yetu na kuhakikisha kombe linabaki nyumbani.”
Kiungo wa Ningeria, Frank Onyeka, anaamini ni muhimu kwa mashabiki kuiunga mkono timu yao. "Tunajua nini kinahitajika ili kushinda Afcon, sare tulizopata katika michezo miwili iliyopita ni somo la kujifunza. Tunahitaji uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki," anasema kijana huyo wa miaka 25.
Nigeria ilitoka katika hatua ya 16 bora nchini Cameroon na Onyeka anatarajia kibarua kigumu katika kundi lao: "Timu za Afrika si rahisi kukutana nazo. Tunapaswa kujiandaa kiakili na kimwili."
Linaundwa na Misri, Ghana, Cape Verde na Msumbij. Misri watasafiri Afrika Magharibi baada ya kupoteza fainali mbili kati ya tatu za mwisho za Afcon - dhidi ya Cameroon (2017) na Senegal (2021).
Mwandishi wa habari wa Misri Inas Mazhar, anasema, "Msumbiji itakuwa timu rahisi kwa kuzingatia tofauti ya uzoefu na historia kati ya timu hizo mbili, lakini mechi ya pili dhidi ya Ghana itakuwa ngumu na muhimu zaidi, Misri itapigana kushinda ili kupata nafasi ya kwanza."
"Licha ya Cape Verde kufuata, Mafarao wana nafasi kubwa ya kumaliza kileleni mwa kundi na kusonga mbele ni jambo la uhakika.”
Kocha Mreno, Rui Vitoria amechukua usukani wa kuongoza timu hiyo mwezi Julai 2022. Haya yatakuwa mashindano yake ya kwanza makubwa akiwa na Misri.
Mtangazaji wa BBC Sport na mwanahabari George Addo Jr anasema, “mashabiki wa Ghana wana wasiwas kuhusu timu hiyo ambayo imeshindwa kufika robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika tangu 2017.”
"Ghana ilitolewa katika hatua ya 16 bora mwaka 2019, na ilishindwa kusonga mbele hatua ya makundi nchini Cameroon," aliongeza.
"Changamoto ambazo timu ilikabiliana nazo zilidhihirika wakati wa mechi za kufuzu. Timu ilikosa muunganiko, benchi la ufundi lilionekana kuyumba katika kuchagua wachezaji, na kutojitokeza kwa wingi mashabiki baada ya kufanya vibaya mara kwa mara.
Ghana ilipata bao la dakika za mwisho kuifunga Madagascar katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia na kisha kushindwa na Comoro, Addo Jr anaamini, "Ghana haina muamana.”
"Mechi dhidi ya Cape Verde na Msumbiji zimekuwa chanzo cha wasiwasi kutokana na uchezaji mbovu wa timu hiyo katika siku za hivi karibuni," anasema.
"Pamoja na hayo, Black Stars itahitaji kuwaingiza wachezaji wao muhimu ili kupata nafasi.”
Linaundwa na Senegal, Cameroon, Guinea na Gambia. Cameroon ni timu kubwa ya uzani mzito barani Afrika, imeshinda Kombe la Afrika mara matano, lakini ilipata nafasi ya tatu nyumbani katika mashindano yaliyopita.
"Tunatarajia wataleta kombe nyumbani. Tulishinda Kombe letu la kwanza la Afrika mjini Abidjan 1984," mchambuzi wa soka wa Cameroon Lawrence Nkede anasema.
Matokeo ya timu hiyo katika fainali za 2021 yaliibua hisia tofauti. Wakati uimara wa timu hiyo ukisifiwa, huzuni ilitanda baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Misri kwa mikwaju ya penalti.
Wafuatiliaji wa soka wana wasiwasi kuhusu kukosekana kwa utulivu katika kikosi cha kwanza cha kocha Rigobert Song. “Katika mechi kumi zilizopita, tumepanga timu kumi tofauti. Ni vigumu sana kuisoma timu na uwezo wake halisi,” Nkede anaeleza.
Huku kipa Andre Onana akionekana kushuka kiwango katika klabu ya Manchester United na mashaka juu ya uwezo wa mshambuliaji Bryan Mbeumo, huenda Simba hao tayari wamejeruhiwa kabla ya mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Guinea kuanza.
Timu ya Taifa Guine imetinga hatua ya 16 bora katika mashindano matatu yaliyopita, huku Gambia ikirejea tena baada ya kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika Afcon.
"Gambia italazimika kujituma vilivyo ili kufuzu baada ya kutocheza vizuri na kushindwa mara mbili katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia," anasema mwanahabari Momoudou Bah.
Kikosi cha kocha Tom Saintfiet kitacheza na Senegal katika mechi ya ufunguzi, ni mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 15 nchi hizo mbili kumenyana katika ngazi ya juu.
Soka la Gambia linakuwa, huku nchi hiyo ikishiriki Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16, lakini Saintfiet amekosolewa kwa falsafa yake ya uchezaji.

Post a Comment