Zelensky afuta ghafla mkutano na Seneti ya Marekani huku kukiwa na mvutano wa ufadhili

 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesitisha mkutano wa hadhi ya juu na wabunge wa Marekani huku kukiwa na mvutano kuhusu ufadhili wa Marekani kwa nchi hiyo siku zijazo.

Alikuwa amepangiwa kufanya mkutano na Bunge la Seneti kwa njia ya Video siku ya Jumanne, lakini ilighairiwa dakika za mwisho.

Ilikuja baada ya afisa wa ngazi ya juu wa Ukraine kuonya kuwa wako katika hatari ya kushindwa vita dhidi ya Urusi ikiwa msaada zaidi wa kijeshi wa Marekani hautapitishwa.

Kiongozi wa Seneti Chuck Schumer hakueleza ni kwa nini Bw Zelensky hakushiriki.

Mwakilishi mkuu wa chama hicho cha Democrat alisema rais wa Ukraine alipata shughuli zingine "dakika ya mwisho", bila kutoa maelezo zaidi.

Mkuu wa wafanyakazi wa Bw Zelensky, Andriy Yermak, alisema mapema Jumanne kulikuwa na "hatari kubwa" ya kushindwa kwa Ukraine bila ya kuendelea kuungwa mkono na Marekani.

"Itakuwa vigumu kubaki katika [nafasi] ile ile na kwa watu kuendelea kunusurika," aliongeza, katika hotuba kwenye Taasisi ya Amani ya Marekani huko Washington DC.

Tathmini mbaya ya Bw Yermak ilitolewa saa chache kabla ya Bw Zelensky kujiondoa kwenye mkutano uliopangwa kwa njia ya video na maseneta wa Marekani ili kuwafahamisha kuhusu juhudi za vita.

Ubalozi wa Ukraine mjini Washington DC haukujibu mara moja swali la BBC lililotaka maelezo zaidi ya kughairi.

Hatua hii inawadia baada ya shinikizo jipya kutoka Ikulu ya White la msaada wa ziada kwa Ukraine. Bunge la Marekani, hata hivyo, bado haliko karibu na makubaliano ya kifurushi cha matumizi ambacho kingesaidia kufadhili juhudi za kukabiliana na vita.

No comments