Israel yasema imepata moja ya hifadhi kubwa ya silaha za Hamas
Jeshi la Israel (IDF) linasema limepata moja ya hifadhi kubwa zaidi ya silaha za Hamas kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ikiwa na mamia ya roketi, maguruneti, ndege zisizo na rubani na vifaa vya milipuko.
Msemaji wa IDF wa vyombo vya habari vya Kiarabu, Avichay Adraee, amesema kuwa silaha hizo zilipatikana karibu na zahanati na shule.
IDF ilidai kuwa imepata mamia ya makombora, makumi ya makombora ya kuzuia silaha, makumi ya vifaa vya vilipuzi, makombora ya masafa marefu ambayo "yaliyopangwa kufyatuliwa katikati mwa Jimbo la Israeli",pampja na makumi ya maguruneti .
“Silaha zote zilikamatwa na vikosi hivyo na baadhi yake zililipuliwa uwanjani huku nyingine zikipelekwa kufanyiwa uchunguzi.
Alisema "miundombinu ya kigaidi ilipatikana karibu na ndani ya makazi ya raia " ikitoa "ushahidi zaidi wa shirika la kigaidi la Hamas kuwatumia wakaazi wa Ukanda wa Gaza kama ngao za kibinadamu za vita"

Post a Comment