Kim Jong Un aangua kilio huku akitoa wito kwa wanawake wa Korea Kaskazini kuzaa watoto zaidi

 

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UN false amewasihi wanawake katika nchi hiyo ya Asia Mashariki wazae watoto zaidi na kuwalea kama "wakomunisti," na kulia alipokuwa akitoa hotuba ya hisia mbele ya hadhira iliyojaa hisia.

"Kukomesha kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa na kutoa matunzo bora ya watoto na elimu ni mambo yetu yote ya kifamilia ambayo tunapaswa kutatua pamoja na mama zetu," Bw Un alisema, akitokwa machozi na kujipangusa kwa leso nyeupe.

Kilio cha Bw Un kimefuatia kupungua kwa viwango vya uzazi nchini mwake.

Wakati wa Kongamano la Tano la kitaifa la Wanawake lililofanyika mjini Pyongyang, Un alielezea kuhusu "majukumu ya utunzaji wa familia," ambayo yalijumuisha wito kwa wanawake kutimiza wajibu wao na kuimarisha mamlaka ya kitaifa kwa kupata watoto zaidi.

"Kuzuia kushuka kwa viwango vya kuzaliwa na malezi bora ya watoto ni majukumu yetu yote ya utunzaji wa familia tunayohitaji kushughulikia tunapofanya kazi na akina mama," alisema Kim Jong Un.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu linakadiria kuwa kufikia mwaka wa 2023, kiwango cha uzazi, au wastani wa idadi ya watoto wanaozaliwa na mwanamke nchini Korea Kaskazini, ilifikia 1.8, huku kukiwa na kushuka kwa kasi kwa kiwango hicho katika miongo ya hivi karibuni.


No comments