Waziri wa Israel aonya Hezbollah kuhusu mashambulizi mpakan

Jeshi la Israel litachukua hatua ya kuiondoa Hezbollah kwenye mpaka na Lebanon iwapo mashambulizi yake yataendelea, waziri wa Israel ameonya.

Benny Gantz alisema IDF itaingilia kati ikiwa ulimwengu na serikali ya Lebanon haitawazuia wanamgambo kufyatua risasi kaskazini mwa Israel.

Wakati wa suluhu la kidiplomasia ulikuwa ukiisha, aliongeza.

Majibizano makali ya risasi yamekuwa yakiongezeka tangu Hamas iliposhambulia Israel tarehe 7 Oktoba.

Hali hii imesababisha wasiwasi kwamba mzozo wa Gaza unaweza kuwa mpana katika eneo lote.

"Hali kwenye mpaka wa kaskazini wa Israel inadai mabadiliko," Bw Gantz aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Jumatano usiku.

Amesema kama dunia na serikali ya Lebanon haitachukua hatua ili kuzuia kufyatuliwa risasi kwa wakazi wa kaskazini mwa Israel, na kuwaweka mbali na mpaka Hezbollah, IDF itafanya hivyo."

Bw Gantz, mwanasiasa wa upinzani na kiongozi wa zamani wa jeshi la Israel, alijiunga na baraza la mawaziri la vita la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kama waziri asiye na wizara maalum kufuatia mashambulizi ya Hamas.

No comments