Mlipuko wa lori la mafuta wauwa zaidi ya watu 40 nchini Liberia

Zaidi ya watu 40 wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kuanguka na kulipuka katikati mwa Liberia, afisa mkuu wa matibabu nchini humo Francis Kateh amesema.

Lori hilo lilianguka kando ya barabara katika mji wa Totota, kilomita 130 kutoka mji mkuu, Monrovia

Liliwaka moto mara baada ya watu kukimbilia eneo hilo kuchukua mafuta kutoka mafuta, walioshuhudia walisema.

Mwanamke mjamzito alikuwa miongoni mwa waliofariki, na baadhi ya miili ilichomeka hadi ikasalia majivu, Dk Kateh alisema.

Akizungumza na kituo cha Super Bongese TV alisema watu 83 wamelazwa hospitalini kutokana na majeraha waliyopata katika mkasa huo wa Jumanne.

Waathiriwa waliokuwa na majeraha mabaya zaidi wamehamishiwa katika hospitali za Monrovia kwa matibabu, Dkt Kateh aliongeza.

No comments