Wazir wa zamani wa Utalii Najib Balala akamatwa kwa tuhuma za ufisadi
Wapelelezi wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi(EACC) nchini Kenya wamemkamata Waziri wa zamani wa Utalii Najib Balala, vyomba ya habari nchini vinaripoti.
Hatua hiyo inafuatia madai kwamba Hazina ya Utalii ililipa kwa ulaghai singi bilioni 8.5 ili kuanzisha tawi la Pwani la Chuo cha Utalii nchini Kenya (baadaye kilipewa jina la Ronald Ngala Utalii College) wakati huo akiwa waziri.
Waziri huyo wa zamani alikamatwa pamoja na wengine watatu akiwemo Leah Adda Gwiyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, na Joseph Odero wa Wahandisi wa kampuni ya West Consult Engineers..
Msemaji wa EACC Eric Ngumbi aliyenukuliwa na vyombo vya habari alisema Bw Balala atasafirishwa hadi Mombasa kutoka Nairobi na baadaye kupelekwa katika mahakama ya Malindi pwani ya Kenya.

Post a Comment