DC Mbinga azindua zoezi ugawaji vitambulisho vya NIDA



Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Ally Mangosongo alizindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya NIDA Pamoja na kukabdihi kwa Watendaji wa kata wakavigawe kwa wananchi katika maeneo yao. Asisitiza zoezi la ugawaji lifanyike kwa wakati na kwa ufanisi ili kila Mwananchi apate kitambulisho chake cha utaifa(NIDA),

Akiwasilisha taarifa ya zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho vya Utaifa (NIDA) Afisa Usajili Mwandamizi wa Mamlaka ya NIDA Wilaya ya Mbinga, *Ibrahimu Patrick Liduke* Alimshukuru *Mhe.Rais,Dkt, Samia Suluhu Hassan* Kwa kutoa fedha nyingi za kununua mitambo ya kisasa pamoja na kadi ghafi ambazo zimesaidia kuharakisha zoezi hilo.

Ambapo Wilaya ya Mbinga ilianza zoezi la utambuzi na kuwasajili wananchi mwaka 2015, Na hadi kufikia Novemba mwaka 2023, mamlaka ya Vitambulisho vya utaifa (NIDA) Mbinga, Imekwisha kuwatambua na kusajili wananchi 185,986 kati ya wananchi 223,654, Hivyo vitambulisho 131,181 vitazinduliwa na kutolewa kwa wananchi hivi sasa na kufikia  idadi ya Vitambulisho 164,275 ambavyo vitakuwa tayari vimetolewa kwa wananchi.

Akizindua zoezi la ugawaji na kuwakabidhi watendaji kata vitambulisho vya NIDA, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga,Mhe.Aziza Mangosongo alimshukuru *Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan* kwa kutenga fedha nyingi ili zoezi la utambuzi na kusajili vitambulisho vya utaifa kwa watanzania lifanyike pasipo gharama zozote pamoja na kuwaruhusu wananchi kupata huduma kwa kutumia namba za NIDA. Vilevile aliwapongeza wananchi kwa kuwa wavumilvu katika kipindi ambacho hawakuwa na vitambulisho vya utaifa (NIDA).

Aidha, Mhe. Mangosongo aliwataka watendaji kata kuvigawa vitambulisho hivyo kwa muda muafaka sambamba na kuwahamasisha wananchi kuchukua vitambulisho hivyo na kuwahimiza kuvitunza kutokana na umuhimu wa vitambulisho hivyo katika kupata huduma msingi mfano utambulisho wa raia popote unapokuwepo, huduma za kibenki, kupata mikopo, ajira pamoja na huduma za mawasili

Vilevile, Alitoa wito kwa wananchi ambao hawana vitambulisho kuendelea kujisajili, Pia Wazazi kuwahamasisha watoto wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kufika ofisi za Nida ili waweze kutambuliwa na kusajiliwa kupata vitambulisho, Alikadhalika kasoro zote zozote zile zirekebishwe mapema sana ili kuondoa usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Alikadhalika, Alitumia nafasi hiyo kuwataka watendaji kata kusimamia na kuhakikisha miradi yote iliyopo kwenye maeneo yao inakamilika kwa wakati, Aidha aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha sikukuu kusherekea kwa upendo amani na utulivu sambamba na hilo aliwaasa madereva kuongeza umakini wa kufuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.

Mwisho, Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika katika ukumbi mdogo wa ofisi ya Mkuu Wilaya Mbinga na kuhudhuriwa na *Mhe.Jonas Mbunda* Mbunge wa jimbo la Mbinga Mjini, Wakurugenzi wa Halmashauri, Kamati ya usalama, Wakuu wa taasisi na idara pamoja na watendaji wa kata na wananchi baadhi.


Imetolewa na,

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Wilaya ya Mbinga.

Disemba 21, Mwaka 2023.

No comments