Simba waipiga Wydad Benjamin Mkapa, yafufua matumaini robo fainali
Timu ya Simba, ikiwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jioni hii wameipiga timu ya pili kwa ubora barani Afrika, Wydad Cansablanca kwa mabao 2-0 na hivyo kufufua matumaini yake ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa.
Ikicheza mchezo wake wa pili wa kimataifa chini ya kocha mpya, timu hiyo ya Dar es Salaam ambayo ndiyo iliyofanikiwa zaidi katika michuano ya ligi hiyo kwa klabu za Tanzania, ilipata mabao yake hayo katika kipindi cha kwanza, yakifungwa na mshambuliaji wake Ossumba Onana.
Kipindi cha pili Simba ilitumia muda mwingi kujilinda, lakini kama kuna mchezaji ambaye anatakiwa kusifiwa, basi ni mlinda mlango wake Ayoub aluyeokoa michomo ya wazi zaidi ya minne.
Ikiwa na alama tano, Simba inahitaji angalau pointi nne zaidi ili iweze kuingia robo fainali yake ya tatu ligi ya mabingwa Afrika ndani ya misimu mitano iliyopita.

Post a Comment