Mkurugenzi Mtendaji Jukwaa la Wazalendo Huru Tanzania aipongeza Serikali


Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania ambaye pia ni Kada mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mwl.Mohamed Mwampogwa maarufu ‘Mwalimu Pogwa Mzalendo tz’ ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita iliyo chini ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo inafanya ya kutoa huduma bora kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa Uhuru kwa Wananchi na Vyombo vya habari katika kutoa maoni,kukosoa na kuishauri Serikali na kusema kuwa hii ni hatua nzuri sana inayo ashiria Utawala bora katika taifa letu.

Mwl.Mwampogwa ambaye ni Muasisi wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania lenye Wanachama karibia 125000 inchini mbalo limejikita katika kutoa Elimu na Hamasa juu ya Agenda ya Uzalendo na kujitolea kwa Jamii amewataka Wajumbe wa Jukwaa hilo kuongeza kasi ya kutoa Elimu ya Uzalendo na kujitolea kwa Jamii hususan maeneo ya Vijijini ambako baadhi ya Wananchi hawatumii Mitandao ya Kijamii.



 Lakini pia amewataka Wajumbe wa Jukwaa hilo kuongeza kasi ya kuzitafsiri na kuzitangaza kazi zote zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Mama yetu Dkt.Samia Suluhu Hassan,Chama tawala na Serikali bila kusahau kukosoa na kuishauri Serikali kuwa wapi hapako sawa na nini kifanyike ili kwa pamoja tulijenge taifa letu kwa Amani na Upendo.

Mwl.Mwampogwa aliyasema hayo tarehe 13.12.2023 alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Redio Dizzim FM iliyopo Mkoani Morogoro hata hivyo amewaelekeza Mwenyeviti na Katibu Mkuu Jukwaa la Wazalendo huru taifa kuwahimiza Viongozi wa Majukwaa ya Wazalendo huru ngazi ya Wilaya na Mikoa kuhakikisha kuwa wanawaongoza Wajumbe wa Majukwaa yao vyema kwa kujadili pamoja na kuweka Program nzuri za kuyagusa makundi maalumu kama Yatima,Walemavu,Wazee,Wajane na Watoto Wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia misaada pamoja na kuihamasisha Jamii kutoa msaada na haki za msingi za makundi hayo ambayo yanaitegemea Jamii yao.

“Katika kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia Wajumbe wa Jukwaa la Wazalendo huru wanapaswa wajitahidi kupinga vitendo vyote vya Ukatili na pia kutoa Elimu kwa Jamii juu ya madhara yanayoweza kuikumba Jamii kutokana na hali hii ya Ukatili lakini pia kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoa taarifa za Ukatili wa Kijinsia na kuhusu suala la kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi Majukwaa ya Wazalendo huru ngazi ya Wilaya na Mikoa yaendeshe Program za kupanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira ikiwemo upandaji Miti” alisema Mwl.Mwampogwa.



Mwl.Mwampogwa ambaye pia ni Msanii wa Muziki wa nyimbo za Asili,Uzalendo na Kizazi kipya nchini amehimiza Wazalendo huru Tanzania kutumia Sanaa mbalimbali kutoa Elimu ya Uzalendo na kujitolea mfano nyimbo zinazotoa Hamasa  ya kutunza Amani na Utulivu wa nchi,kufanyakazi,kutunza Mazingira nk lakini pia kutoa Elimu ya Ulipakodi,Ulinzi wa Rasilimali za taifa na Usalama Barabarani.Lakini pia amesisitiza Wazalendo kuungana na kuandika Vitabu vya Mashairi na Tenzi kama sehemu ya kukuza Lugha yetu ya Kiswahili na pia kulinda Utamaduni wetu nchini.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi amewahimiza Wazalendo huru kuendelea kujisajili katika Orodha ya Wazalendo huru waendao katika Sherehe za Mapinduzi Zanzibar tarehe 12.01.2024."Sherehe zile ni muhimu sana kwetu sisi Wazalendo huru Tanzania kwani ni sehemu ya kumuenzi Mzee wetu Sheikh Abeid Aman Karume na wenzake kwa kuongoza harakati zilizo liweka huru Taifa letu kwa upande wa Tanzania Visiwani (Zanzibar) hivyo tukaungane na ndugu zetu kuadhimisha siku hii adhimu katika nchi yetu,lakini pia tunawashukuru sana Viongozi wetu wa Chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango wao mkubwa wanao lipatia Jukwaa hili" alimalizia Mwl.Mwampogwa

Hata hivyo mwaka 2024 Mwalimu Mwampogwa anatarajia kuzindua kitabu chake cha Mashairi kiitwacho “Diwani ya Mwalimu Mwampogwa” Diwani ambayo itapambwa na Mashairi na tenzi zinazohusu au kuzungumzia agenda ya Uzalendo na kujitolea nchini.

No comments