Kuingia bure kwa sharti la jezi ya Yanga ni batili
Sawa.
Uamuzi wa bosi Ghalib ni mzuri kwa klabu yake, kwa mashabiki wake na pengine,
kwa watu wengi wa mpira. Ule mzunguko pale Uwanja wa Taifa, ndiyo unaobeba
mashabiki wengi zaidi kuliko maeneo mengine yote ya kukaa.
Unapozungumzia
Uwanja wa kubeba watu 60,000 wakiwa wamekaa, sehemu ile ya MZUNGUKO, inaweza
kubeba takribani ya asilimia 80 ya watu hao.
Soka
ni mchezo wa mashabiki. Kuna watu wanapenda kuangalia mpira, lakini hawana timu
wanayoishabikia, kwao burudani ni soka. Basi.
Kati
ya hawa wasio na timu, wengi hukaa eneo hilo la mzunguko. Na tukumbuke, mechi
ya kesho kati ya Yanga na Madeama, siyo mali ya miamba hawa wa Jangwani. Hii ni
mechi ya CAF.
Yanga
kuibeba na kuifanya yao, siyo sawa. Hii si mechi ya Wiki ya Wananchi, ambapo
klabu ingeweza kufanya itakavyo.
Unamlazimishaje
shabiki wa mpira avae jezi ya klabu kama sharti la kuingia uwanjani?
Mechi
hizi zina viingilio, weka kiingilio watu wa mpira waje uwanjani, mtu ashindwe
kiingilio. Unataka kusema nini kwa mashabiki wa Madeama waliopo hapa nchini,
wavae jezi za Yanga ndipo waingie?
Ni
vyema mamlaka zinazohusika zikaingilia kati suala hili.
Ni
kweli, mashabiki wengi wa Yanga ndiyo watakaojitokeza, lakini vipi mashabiki wa
mpira wanaoshabikia Simba, Coastal, Azam na Namungo?
Nasisitiza,
hii siyo mechi ya Bonanza la Yanga, hii ni mechi mali ya CAF, ila Yanga
wanachezea nyumbani. TFF, kama mwakilishi wa shirikisho la soka Afrika, fanyeni
jambo kwa faida ya mashabiki wote wa mpira!

Post a Comment