Mtoto wa Sheta aukwaa Uenyekiti Chipukizi Taifa

Qaillah Nurdin, mtoto wa msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sheta. jana alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi, uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma.

Qaillar ambaye namba yake ya uchaguzi ilikuwa ni moja, alipanda jukwaani na kuomba kura kwa kujiamini sana, akitoa ahadi lukuki za nini atafanya kama atapewa nafasi hiyo.

Akionekana kuongea mambo makubwa kuliko umri wake, binti huyo alishangiliwa mno wakati akiomba kura, hali iliyowalazimu wasimamizi wa uchaguzi huo kuingilia kati, wakiwakumbusha kuwa hawapaswi kufanya hivyo kwani kinyume na taratibu ya uchaguzi.

Kama.moja ya chombezo wakati akiomba kura, alisikika akisema 'Kwa mujibu wa majina niliyopewa na wazazi wangu, bila kushirikishwa...naitwa Qaillar Nurdin...

No comments