Tumieni fursa mnazozipata kuwa chachu kwa wanawake wengine--Katibu CCM Pwani
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani *ndg Bernard Ghaty* leo tarehe *21/12/2023* amewataka wanawake viongozi kutumia fursa wanazozipata na kuwa chachu kwa wanawake wengine katika Taifa la Tanzania.
*Ghaty* ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa wanawake waliohudhuria mkutano wa Wanawake Vijana wa Afrika ulioandaliwa na taasisi ya YOUNG WOMEN OF AFRICA iliyojumuisha mataifa 16 ya Afrika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kibaha Mjini.
Amesema kila mwanamke Kiongozi anatakiwa kutumia nafasi alionayo kuwanufaisha wanawake wenzake katika nyanja mbalimbali.
*Ghaty* amesema wanawake wanatakiwa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa 2024 kwani *Mhe, Dr. Samia Suluhu* *Hassan Raisi wa Jamhuri* *ya Muungano* *wa Tanzania* ameboresha sana maeneo ya afya, barabara, shule na kumekuwa na mahusiano mazuri sana kati ya Chama na Serikali.
Aliipongeza sana UWT Taifa chini ya Mwenyekiti wake *Mary Chatanda* kwa kazi wanazozifanya na kuonyesha uhai wa Jumuiya.
Amesema wako wanaokanyaga katiba ya CCM kwa kukiuka utaratibu, Kanuni na miongozo hivyo amewataka kuwa makini katika utendaji wao.
*" Acheni kuwaza uchaguzi wa 2025 badala yake wazeni uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024"* amesema Ghaty.
Ameendelea kusema kuwa wako viongozi wanaowaza ubunge na udiwani, amewaasa kuacha mara moja tabia za kubeba wagombea hewa wanaovunja taratibu za Chama.
Amehitimisha kwa kumpongeza *Profesa* *Marcelina Chijoriga* Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwaruhusu wanawake hao kufanya mkutano huo wa siku tatu chuoni hapo kabla ya kukabidhiwa vyeti katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kibaha Mjini.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Pwani David Mramba amewataka wanawake hao kuzidi kumuunga mkono *Mhe, Daktari Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa* *Tanzania* katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM *2020-2025.*
Mramba amewaeleza wanawake hao kuzidi kujiendeleza kielimu ili wanapogombea nafasi mbalimbali kusiwe na vikwazo vya elimu.
Pia amewataka kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuhakikisha wanawashawishi wanawake wenzao kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi.
Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani *Bi Fatuma Ndee* amewapongeza wanawake hao kwa kuhudhuria mkutano huo ambao umewajenga kifikra na kubadilishana uzoefu kutoka Katika mataifa mbalimbali.
Amesema ni rahisi wao kupata uzoefu wa kibiashara na kiungozi ambapo itawasaidia wao kukua zaidi na kufikia viwango vya juu.
Aidha amesema wapatapo fursa kama hizo za mialiko wawe tayari muda unaofaa na usiofaa kwa ajili ya maslahi ya Jumuiya ya Wanawake na wao binafsi.
Taarifa hii imeandaliwa na:
David Mramba
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM
Mkoa wa Pwani.

Post a Comment