Mechi ya Yanga sasa saa kumi

Mechi ya mzunguko wa nne Ligi ya Mabingwa barani Afrika kati ya wawakilishi wa Tanzania, Young Africans dhidi ya Madeama ya Ghana, sasa utapigwa saa kumi jioni, dimbani Benjamin Mkapa.

Awali mchezo huo ambao piga ua garagaza Yanga inapaswa kushinda, ulikua uchezwe saa moja usiku.

Yanga inashika nafasi ya mwisho katika kundi lake ikiwa na pointi mbili baada ya mechi tatu. Endapo itapoteza mchezo huu itakuwa imetolewa katika mbio za kuelekea robo fainali.

No comments