Mjumbe wa Baraza UVCCM Taifa ataka viongozi kuheshimiana kukijenga Chama
*📍 UVCCM RUNGWE 📍*
Leo Tar 17/12/2023 Jumuiya ya Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Rungwe Imefanya Kikao Cha Baraza la Kikanuni Ambalo Limeongozwa na Mwenyekiti Wa Uvccm Wilaya ndugu. Antony Mwangomo.
Aidha katika kikao hicho ndugu. Timida Fyandomo Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Kuwakilisha Mkoa Wa Mbeya Ndiye Aliyekuwa Mgeni Rasmi wa Baraza, Na Mjumbe Halali wa Baraza Hilo
Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Amendelea na Zoezi La Ugawaji wa T-shirt za Chama na Ametoa T-shirt *150* kwa Wajumbe wa Baraza Hilo.
Aidha Mgeni Rasmi Amewapongeza Wilaya Ya Rungwe kwa Kuendelea Kukipigania Chama na Kuendelea Kukipambania Chama na Serikali Yetu.
Na kuwahimiza Kuendelea Kushiriki Vikao Vyote vya Ndani ya Jumuiya na Chama
Sambamba na Hilo Amehimiza Siasa ya Uchumi kupitia kubuni Miradi Mbalimbali katika Ngazi ya Tawi Hadi Wilaya.
IMETOLEWA NA IDARA YA HAMASA NA CHIPUKIZI WILAYA.
*#UVCCMMKOAWAMBEYA.
#SisinaMamaMLeziwaWana.
#AlipoMamaVijanaTupo.
#2025TuponaMama* .

Post a Comment