Mawasiliano Dar es Salaam na Bagamoyo yakatika
Daraja la Mto Mpiji ambalo lipo mpakani na linalounganisha Wilaya ya
Bagamoyo na Mkoa wa Dar es salaam limefungwa kutumiwa na Waendesha
magari na vyombo vingine vya usafiri baada ya sehemu ya daraja hilo
kutitia na kupelekea uwepo wa shimo kubwa ambalo linahatarisha usalama
wa Watu.
Kwa sasa wanaoruhusiwa kupita kwenye daraja hili ni Watembea kwa miguu
pekee na kama una gari lako au usafiri mwingine utalazimika kuuacha
upande wa pili na kupita hapa kwa miguu.
Tayari Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule na Vyombo vingine vya
ulinzi na usalama vipo hapa darajani ili kuimairisha ulinzi na usalama.

Post a Comment