Chama, Kapama wasimamishwa Simba

Clatous Chota Chama 'Tripple C' pamoja na Nassor Kapama wamesimamishwa katika kikosi cha Simba kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambaa mitandaoni jioni hii, ambayo imetolewa na Meneja wa Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, wachezaji hao watapelekwa Kamati ya nidhamu ya klabu hiyo kwa ajili ya hatua zaidi.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijafafanua nini hasa Mwamba huyo wa Lusaka na Kapama wamefanya, ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuhusika kikamilifu kwenye ushindi wa Simba wa mabao 2--0 dhidi ya Wydad Cansablanca katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

No comments