Shakira alipa Bil. 18.7 kumaliza utata wa kodi Hispania
Mwimbaji nyota wa muziki duniani, Shakira ambaye ni raia wa Colombia, amefikia makubaliano na waendesha mashtaka wa Uhispania kutatua kesi ya ulaghai wa kodi, wakati kesi yake ilipokaribia kuanza na kulipa kiasi cha dola milioni 7.5 zawa na fedha za kitanzania zaidi ya bilioni 18.7.
Mwimbaji huyo wa Hips Don't Lie alikabiliwa na madai ya ulaghai wa kodi ya kiasi cha €14.5m (£12.9m) katika mahakama ya Barcelona.
Waendesha mashtaka wa Uhispania walitaka kumfunga jela miaka minane na kumtoza faini ya euro milioni 23.8 ikiwa angepatikana na hatia.
Shakira, ambaye mara kwa mara amekanusha makosa yoyote, aliamua kuafikiana na uoande wa mashtaka "kwa maslahi ya watoto wangu moyoni".
Aliongeza "hawataki kuona mama yao akisalimisha ustawi wake wa kibinafsi katika vita hivi".
Msanii huyo hapo awali alikataa mpango uliotolewa na waendesha mashtaka, badala yake akachagua kwenda mahakamani.

Post a Comment