Nyota wa zamani wa Raga Afrika Kusini, Hannes Strydom: afariki kwa ajali ya barabarani
Mchezaji nyota wa zamani wa raga wa Afrika Kusini Hannes Strydom amefariki dunia katika ajali ya barabarani akiwa na umri wa miaka 58.
Alikuwa sehemu ya timu ya Springbok ambayo ilishinda Kombe la Dunia la Raga la 1995 baada ya kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mnamo 1994.
Strydom aliichezea Springbok mechi 21 katika taaluma yake kati ya 1993 na 1997.
Mchezaji mwenzake wa zamani na rafiki wa karibu Kobus Wiese aliambia vyombo vya habari vya ndani kwamba maelezo ya ajali bado hayajaeleweka, lakini gari alilokuwa akisafiria Strydom liligongana na teksi ndogo.
Ajali hiyo ilitokea Jumapili karibu na mji wa uchimbaji madini ya makaa ya mawe wa eMalahleni katika jimbo la Mpumalanga.

Post a Comment