Burna Boy na Rema washinda tuzo za kwanza za Billboard Afrobeats
Nyota wa Nigeria Burna Boy sasa ana Tuzo ya Muziki ya Billboard ili kuongeza kwenye mkusanyiko wake wa Tuzo unaoongezeka
Mwimbaji huyo, ambaye alishinda tuzo yake ya kwanza ya Grammy mapema mwaka huu, ametajwa kuwa muigizaji bora wa Afrobeats na Billboard nchini Marekani.
"Hii ni maalum kwa Afrika na kila msanii anayetoka Afrika sasa," alisema akipokea tuzo hiyo Jumapili.
Billboard ndio chombo kipya zaidi cha kuongeza kitengo cha Afrobeats, inayoakisi umaarufu mkubwa wa aina hiyo kimataifa.
Akizungumza katika ujumbe wa video uliorekodiwa,Burna Boy alisema "wakati ujao ni mzuri... Hii ni ncha tu ya barafu lakini mtaona ruwaza yote hivi karibuni".
Msanii mwenzake wa Nigeria Rema pia alitambuliwa katika hafla hiyo kwa kwa wimbo wake unaofahamika karibu kila mahali Calm Down, ambao umevunja rekodi nyingi za chati.
Akikubali tuzo ya wimbo bora wa Afrobeats siku ya Jumapili, Rema aliwashukuru mashabiki wake na kuita tuzo hiyo "sherehe ya umoja na utawala wa kimataifa wa Afrobeats".

Post a Comment