Oscar Pistorius kuachiliwa huru kutoka gerezani kwa msamaha
Bingwa wa zamani wa Olimpiki ya walemavu Oscar Pistorius ataachiliwa kutoka jela kwa msamaha, takriban miaka 11 baada ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Alimpiga risasi Steenkamp mara nyingi kupitia mlango wa bafuni Siku ya Wapendanao mwaka wa 2013, baadaye akidai alidhani kuwa ni mwizi.
Pistorius, ambaye sasa ana umri wa miaka 37, alihukumiwa na mahakama ya Afrika Kusini mwaka 2016 kutumikia kifungo cha miaka 13 jela.
Bodi ya kuwaachilia wafungwa kabla ya kutimiza hukumu yao imepanga kuachiliwa kwake tarehe 5 Januari 2024.
Mama yake Steenkamp hakupinga dhamana lakini - katika barua iliyotumwa kwa bodi ya msamaha - alisema anashangaa iwapo "maswala makubwa ya hasira" ya Pistorius yalishughulikiwa kweli gerezani, na kuongeza kuwa "angekuwa na wasiwasi kwa usalama wa mwanamke yeyote" ambaye sasa anakutana naye.

Post a Comment