Barafu kubwa zaidi duniani yaanza kusongea baada ya miaka 30
Barafu kubwa zaidi duniani iliyokuwa katika eneo moja kwenye sakafu ya bahari kwa muda wa miaka 30 imeanza kusongea.
Barafu hiyo iliyopewa jina laA23a, iligawanyika kutoka ufuo wa Antarctic mwaka wa 1986. Lakini ulitua kwa haraka kwenye Bahari ya Weddell, na kuwa, kisiwa cha barafu.
Ukubwa wake ni karibu kilomita za mraba 4,000 (maili za mraba 1,500) yaani zaidi ya mara mbili ya mji wa London.
Mwaka uliopita umeshuhudia barafu hiyo ikisongea na kwa sasa inakaribia kumwagika kupita maji ya Antaktika.

Post a Comment