Obi Mikel alalamikia familia za wachezaji Afrika

 

Kiungo wa zamani wa Chelsea na Nigeria, John Obi Mikel amedai Waafrika wengi waliofanikiwa kiuchumi wanakumbana na presha kubwa kutoka kwa Familia wakitakiwa kutoa msaada wa fedha kwa lazima na wasipofanya hivyo wanaonekana wabaya na wengine wanapewa vitisho.

Anasema "Hatuzungumzi sana kuhusu hili lakini linawaharibu Wachezaji Kisaikolojia, ukipata fedha zinakuwa sio zako ni za ndugu, Binamu na wengineo, ni tamaduni isiyofaa, tuwaambie wachezaji wanaochipukia kuwa wanatakiwa kuwa imara na maamuzi ya fedha zao.”

Anadai alikuwa mhanga wa hali hiyo kuanzia alipoanza kufanikiwa kisoka, miaka mitano iliyopita aligeuka kuwa adui kwa ndugu baada ya kusitisha kutoa fedha.

No comments