MWENYEKITI CCM PWANI AWATAKA VIONGOZI KUJENGA UHUSIANO MZURI NA WANANCHI

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani NDG Mwinshehe Mlao amewataka Viongozi wa Chama na Serikali ngazi za Wilaya kuhakikisha wamejenga mahusiano mazuri na wananchi ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

NDG Mlao amesema kuwa Kila mmoja awe mfano kwa mwenzake katika kusemeana mambo mazuri ili kutengeneza UMOJA katika kutekeleza ILANI ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.


Ameendelea kusema kuwa mahusiano ya Viongozi kwa Viongozi yatapelekea kuwapa Imani wananchi katika kushughulikia matatizo yao.

Amesema huu ni wakati wa kuondoa tofauti zilizopo ili kurejesha heshima ya Chama na Serikali, huku akisisitiza kuwa hakuna haja ya kugombea fito wakati tunajenga nyumba Moja.


Alimalizia kwa kuwaagiza Viongozi hao kwenda katika maeneo yao kuongeza wigo wa mahusiano na wananchi.

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani NDG Bernard Ghaty amesema ni vigumu sana kuitenganisha CCM na Serikali katika kutekeleza na kuisimamia ILANI ya CCM.

Aidha amewataka Viongozi hao kuwa na tabia ya kupongezana pale mmoja wao anapofanya vizuri ili kuendeleza chachu ya kufanya vizuri zaidi.


Mwisho amemalizia kwa kuwaasa viongozi kuwa na mazoea ya kuvaa sare za Chama kwenye vikao ili kuleta taswira halisi ya Vikao husika.


 Taarifa imetolewa na


David Mramba

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, 

Mkoa wa Pwani.

No comments